(Usiku wa cheo)Lailatu Al-qadr

Kwanini ukaitwa usiku wa cheo (usiku waheshima)? 1. Kumesemwa: Ni kwasababu ya kuutukuza, kama ilivyo kaulu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na (Mayahudi ) hawakumhishimu Mwenyezi Mungu kama inavyotakiwa kumhishimu} (Al-An-a’m – Aya 91).

Na maana yake: Ni kwamba huu usiku ni wenye hishima; kwa kuteremshwa Qur’ani ndani yake na kupatika na kushuka malaika, na ni usiku wa baraka na rehema na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

2. Inasemekana: Al-qadr kwa maana ya kubanika kwa kuwa ndogo sana, kama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: { na yule ambaye amepungukiwa riziki yake (riziki yake imebanika kwa kuwa ndogo sana), atoe katika kile alichopewa na Mwenyezi Mungu} ( At-twalaq – Aya 7).

Na maana ya kubanika kwa kuwa ndogo sana: Ni kule kufichika katika elimu za watu kutambua hasa usiku huo ni usiku wa tarehe ngapi.

3. Na inasemekana: Al-qadr kumaanisha makadirio, kwa maana: katika usiku huu ndiyo kunakadiriwa hukumu za mwaka ulioko; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: { Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hikima} (Ad-Dukhan – Aya 4).

Fadhla za Lailatul.Qadr na Hadhi yake 1. Katika usiku huu ndio Qur’ani iliteremshwa. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Tumeiteremsha (Qur’ani) katika Laylatu-Qadr (usiku wenye hishima kubwa)} (Al-qadr –Aya 1).

2. Usiku huu ni bora kuliko miezi elfu moja. Mwenyezi Mungu U Amesema kuhusu usiku huu: {Huo usiku wa hishima ni bora kuliko miezi elfu }. (Al-qadr –Aya 3).

Yaani matendo ndani ya usiku huu ni bora kuliko matendo ya miezi elfu ambayo hayako katika usiku huu wa hishima.

3. Huteremka Malaika na Jibril katika Usiku huo. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Huteremka Malaika na roho katika usiku huo } [Al-qadr –Aya 4]. Na makusudio ya roho: Ni Jibril.

Kutoka kwa Abu Hureira t Anasema: Amesema Mtume (saw): (Lailatu Al-qadr ni tarehe ishirini na saba au ishirini na tisa, hakika Malaika usiku huo ni wengi sana katika ardhi kuliko idadi ya changarawe za mawe) [Fat-hul-Baary (4/255).].

4. Ni usiku wa amani. Anasema Mwenyezi Mungu U: { Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri } (Al-qadr – Aya 5).

Yaani usiku wote huo ni kheri tupu, hakuna shari kutoka mwanzo wake hadi kupambazuka kwa alfajiri.

5. Ni usiku wenye baraka. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwa yakini tumeteremsha (Qur’ani) katika usiku uliobarikiwa – bila shaka Sisi ni waonyaji} (Ad-Dukhan – Aya 3).

Ibn Abbas t Asema: ”Yaani: Usiku wa Lailatu Al-qadr”.

6- Ndani ya usiku huu ndiyo yanakadiriwa makadirio ya mwaka mzima. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hikima} (Ad-Dukhan – Aya 4).

7. Atakayesimama kufanya ibada katika usiku huu hali ya kuamini na kutarajia malipo atasamehewa madhambi Amesema Mtume (saw): (Atakayesimama (kufanya ibada) usiku wa Lailatu Al-qadr kwa imani na kutarajia malipo, basi atasamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi yake) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

viungo vya nje edit

cheo cha usiku

[1]