Zaaka ya (vitu) vinavyotoka ndani ya ardhi

Maana ya Vinavyotoka kwenye Ardhi Vinavyo toka Ardhini Kila kinachotoka ndani ya ardhi, na kinawezekana kunufaika nacho.

Kinachotoka ndani Ardhini ni Sampuli mbili: ni Nafaka na Matunda na Madini, na Hazina iliyozikwa Ardhini

Kwanza: Nafaka na Matunda Maana ya Nafaka na Matunda Nafaka Kila tembe (mbegu) inayohifadhiwa katika mtama, ngano na mfano wa hii.

Matunda Kila tunda linalohifadhiwa kama tende, na zabibu, na lozi.

Hukumu ya kutoa Zaka ya nafaka na matunda Zaka ya nafaka na matunda ni wajibu, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: {Na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake} (Al-An-am: 141);

na kwa kauli ya Mtume (saw): (Kwa yaliyo nyunyiziwa (maji) ya mbinguni (yaani mvua) au mito au kama yamemea yenyewe [ Yamemea yenyewe: Ni mavuno yaliyomea kwa kunywa maji bila ya kunyunyuziwa maji, ima ni kwa unywevu wa mizizi yake kuwa na umajimaji au kupitia kwa mvua na umajimaji (kama vile hali ya umande) na mito.] (inafaa mtu atoe) ushuri moja (yaani atoe sehemu moja kwa kumi ya mavuno atakayopata (1/10), na yaliyonyunyiziwa kwa kumwagiwa maji [ Yaliyonyunyiziwa kwa kumwagiwa maji (na mtu mwenyewe): Yaani amemwagia maji na akagharamika katika kuyatoa hayo mavuno.] nusu ushuri (yaani atoe sehemu moja kwa tano yamavuno atakayopata (1/20)” [ Imepokewa na Bukhari.].

Masharti ya kuwajibika kwa Zaka ya nafaka na matunda 1.Iwe ni katika (mavuno) yanayohifadhika. Ikiwa si mavuno ya kuhifadhika, na ni mavuno ya chakula chake cha siku basi hakuna Zaka ya kutolewa hapo; kwasababu sio ya kuhifadhiwa hayakuzidi mahitaji yake ya kula kwake kwa kila siku, hivyo basi hayamtoshelezi mahitaji yake; kwa kukosekana utulivu wa kunufaika (na yale mavuno).

2. Iwe ni (mavuno) yanayopimwa. Na hii iwe ni katika (mavuno) yanayopimwa kwa mizani ili kulinganishwa na saaq, nayo ni kipimo (fulani), hii inaashiria kutambulika kwa mavuno hayo; kwa kauli ya Mtume (saw): (Hakuna katika nafaka, wala tende Zaka yoyote mpaka ifike saaq tano [Al - Wasaq: Ni Sawa na Pishi 60.] ) [Imepokewa na Muslim.].

Basi ikiwa sio mavuno yanayopimwa kama vile mboga, na mabogaboga, hakuna Zaka kwa vitu hivi.

3. Iwe imemea kwa kupandwa na mtu katika Ardhi yake. Ama yaliyomea peke yake bila kupandwa na mtu Mavuno hayo hayana Zaka.

4. Mavuno yafikie Nisabu. Nayo ni Makapu matano, kwa kauli ya Mtume (saw): (Hakuna katika nafaka wala tende Zaka yoyote mpaka ifike saaq tano) [Imepokewa na Muslim.],

na hii itakuwa ni swaa’(Pishi) mia tatu, nayo ni sawa na (612kg) katika ngano nzuri, na yanachanganywa matunda ya aina moja pamoja ya mwaka mzima ili kukamilisha nisabu; kama sampuli tofautitofauti za tende, kwa mfano tende za sukkari zinachanganywa na tende za barhy, kwasababu ni sampuli za mavuno aina moja, wala haifai kuchanganya aina tofauti ya mavuno kwa nyengine, hivyo basi haifai kuchanganya ngano kwa shayir, wala ngano kwa tende.

Wakati wa kuwajibika kutoa Zaka ya Nafaka na Matunda. Inawajibika utoaji wa Zaka katika nafaka pindi pale zitakapokomaa kuwa tayari, na katika matunda pale yatakapoanza kuonesha uzuri wake, kwa hali ya kwamba yamefikia kuwa mazuri kulika, na atakayeuza matunda au nafaka baada ya wakati wake wa kuwajibika kutolewa Zaka basi Zaka itakuwa ni kwa aliyeuza, kwasababu alikuwa akimiliki mavuno hayo wakati ule wa kuwajibika kutolewa Zaka.

viungo vya nje edit

zaka ya vitu

[1]