Maana ya zaka za fitri Zaka ya fitri Zaka aliyoifaradhisha Mtume (s.a.w)wakati wa kufungua katika kumalizika kwa mwezi wa Ramadhan.

Na imeitwa Zaka ya fitri kwasababu inawajibika pale mtu anapofungua kwa kumalizika mwezi wa Ramadhani.

Hukumu ya Zaka ya Fitri Zaka ya Fitri ni lazima kwa kila Muislamu anayemiliki siku ya Idi na usiku wake pishi ya chakula cha ziada ya chakula chake cha siku na cha familia yake (nayo ni karibia kilo mbili na nusu).

Na yamlazimu mwenye kutoa Zaka ajitole Zaka nafsi yake, na mke wake, na wale ambao ni jukumu lake kuwalisha, hata mtoto alioko kwenye tumbo la mamake. Na dalili ya kuwajibika kwake ni ilivyopokewa kutoka kwa Ibn Umar radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie asema: (Amefaradhisha Mtume (s.a.w) Zaka ya Fitri Pishi moja ya tende, au Pishi moja ya Shayir (aina ya nafaka) kwa mtumwa na muungwana, na mume na mke, na mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha itolewe kabla ya watu hawajatoka kwenda kuswali (Idd) [Imepokewa na bukhari na muslim.].

viungo vya nje edit

zakah ya fitri [1]