Baba yetu
The Lord's Prayer in Swahili (Kiswahili Bible CLT)
editMathayo 6:9-13
9 Basi, hivi ndivyo mnavyopaswa kusali: ‘Baba yetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe.
10 Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
11 Utupe leo chakula chetu cha kila siku.
12 Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.
13 Usitutie katika majaribu, lakini utuokoe na yule Mwovu.’ [ Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
The Lord's Prayer in Swahili (Catholic Version)
edit- Baba Yetu uliye mbinguni,
- Jina lako litukuzwe;
- Ufalme wako uje,
- Utakalo lifanyike
- Duniani kama mbinguni.
- Utupe leo mkate wetu wa kila siku,
- Utusamehe makosa yetu,
- Kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
- Usitutie katika kishawishi,
- Lakini utuopoe maovuni.
- Amina.