Page:Swahili tales.djvu/102

This page has been proofread.
82
SULTANI DARAI.

kosi kenge, na wa tatu hamkosi nyoka, na la nne akali ya kitu ni vyura, nao huuma watu, nami hivi vyote naviogopa. Bassi bwana, koga papa hapa mtoni.

Bwana wake akiingia katika mto, akaoga. Akamwambia, jisugue sana na udongo. Akamwambia, utwae mchanga, uyasugue meno yako sana kwa mchanga, kwani meno yako yana ukoga. Akajisugua kwa udongo sana, akasugua meno kwa mchanga sana. Akamwambia, haya bassi, toka, jua limekuchwa, twende zetu.

Akileta pale zile nguo, akamwambia, Fungua, bwana. Akafungua zile nguo, akavaa. Akavaa kikoi seyediya, akavaa na kanzu doria, akajifunga na jambia la temsi la thahabu, akavaa na joho yake nyeusi, ilio njema sana, akajipiga kilemba kariyati, kitambi kilicho chema sana. Akavaa na viatu, akitia kitara kwapani, akashika bakora mkononi ya mtobwe.

Akamwambia, Bwana! Akamwambia, Lebeka mwanangu, lebeka mfathili wangu, lebeka mzishi wangu, lebeka msemaji wangu, lebeka nuru yangu. Akamwambia, huko tunakokwenda usitoke na neno, liwa lo lote katika kinwa chako, zayidi ya kuamkiana na kutakana habari, usizidi neno tena, maneno yote niache mimi, huna lako neno kutia. Akamwambia, Vema. Akamwambia, Huko mimi mimekuposea mke, na mahari, na nguo, na mikaja, na vilemba, na ubeleko, na jamii za ada za mke na za mamaye, na za babaye pia nimewapa. Akamwambia, mimi sitanena kitu. Akamwambia, bass, panda fras, twende zetu.

Paa akaenda mbio, akasimama mbali, akamwambia, bwana, bwana! Akamwambia, labeka. Akamwambia,