Page:Swahili tales.djvu/118

This page has been proofread.
98
SULTANI DARAI.

chafya, chééé. Mzee yule akafurahi sana, akamwona yule paa akienda chafya. Akampepea sana, akamtia maji sana, na kumgeuzageuza, hatta paa akaondoka.

Yule bibi akasema, ah! mjukuu wangu wee, pole mwanangu, wala sikukuthania kama uta'mweza huyu. Akamwambia, mama, nalitangulia kukwambia, masifiwa sikuona shani, nda kujionea. Akamwambia, kweli, mwanangu, akamwambia, kwani nimeona.

Akamwambia, njema unipe habari. Akamwambia, kama ipi, mwanangu? Akamwambia, hapana pingamizi tena mbele yetu? Akamwambia, mbele kweu na nyuma kweu, sijui ya Muungu. Bassi nataka unionya nyumba hii, mwanzo hatta mwisho, chini hatta juu, ndani hatta nje. Akamwambia, Ee walla, baba. Akamwambia, kwanza na tupite uani. Akamwambia, nitakupitisha, baba, kwenda kukuonya cha siri na cha thahiri zalizowekwa. Akamwambia, vema, mama yangu, zema haziozi. Akamwambia, kweli, mwanangu.

Bassi tena akamwonya ghala za mali, akamwonya na vyumba, vilivyotiwa vyakula vya mali. Akamwonya na vyumba vilivyotiwa watu wazuri, waliofungwa tokea zamani. Akampandisha hatta orofani, akamwonya kama kilichomo kinenacho na kisichonena. Hizi, bwana, mali zako. Akamwambia, Mali haya yaweke wewe, hatta mimi hamwite bwana wangu, ndiye mwenyi mali haya.

Yule paa akafurahi sana. Ile nyumba imempendeza sana, na atakapokuja yeye na mkwewe, na mkewe, na jamii ya watu watakaofuatana nao, killa atakaokuja, akiona nyumba hii, atanena hii ndio nyumba, bassi, kwani kule mji wao hakuna nyumba yapatao nusu ya ile. Ah! bassi, paa