Page:Swahili tales.djvu/132

This page has been proofread.
112
SULTANI DARAI.

nyumba kama hii. Na atakayokwambia iko nyumba zayidi kuliko hii, mtu huyo ni mwongo, na mtu atakayokwambia, yuko mtu mwenyi akili na busara, na kujua makazi ya wangwana na watumwa, na kujua, huyu mkubwa na huyu mdogo, akupitaye wewe, mtu huyo mjua kuwa mwongo. Akiwa akitokea wa kwanza huwa huyu, wa pili ni wewe. Na mtu atakaokwambia zayidi, mwambie kuwa mwongo.

Wakikaa siku nyingi katika ile nyumba, hatta wakaomba rukusa, wale waanaake, Twataka kwenda kwetu. Akawaambia, Ee, wangwana wangu, ehee, bibi zangu, ee seyidi zangu, mmekuja jana ussubui, leo jioni mtaondoka? Wakamwambia, Tumekuja siku nyingi, baba, tumemleta harrusi kwa mumewe, nasi tumefika salama, nasi twataka kurudi, tukatazame shauri ya kwetu. Akawaambia, Ee walla, bibi, Ee walla bibi zangu, Ee walla, na jamaa zangu.

Akawafanya zawadi nyingi, akawapa wale wangwana, akawapa zawadi nyingi, akawapa watumwa wa wale wangwana. Wangwana wale wakafurahi sana, na wale watumwa wakafurahi sana kwa zawadi walizopewa. Wakamwona yule paa ni bora marra elfu kuliko yeye, bwana wake, Sultani Darai. Wakatoka, wakaenda zao kwao. Akawapa na watu wakawasindikiza.

Wakakaa kitako, paa na bwana wake, katika nyumba, muhulla wa siku nyingi.

Paa akanena na bibi yule kizee, Mimi nimekuja na bwana wangu katika nyumba hii, katika mji huu, nami nimemfanyia mambo mengi bwana wangu, tena mambo mema, tena mambo ya kumwinua uso wake mbele za watu, hatta tumefika hapa, hatta leo hajaniuliza, Je! baba, je!