Page:Swahili tales.djvu/138

This page has been proofread.
118
SULTANI DARAI.

Akamwambia, nimekwenda hatta darini nnamkuta bibi na bwana, wamekaa kitako katika kitanda cha mawe ya marmari, na godoro kitambaa cha mdarahani, na takia huku na huku, wanatafuna tambuu, mke na mume. Akaondoka bwana, akaniambia, umekuja taka nini, kizee? Nikamwambia, nimetumwa na mtumwa wako paa, kuja kukwambia kama hawezi. Yule mkewe akaruka, akaisha akasangaa, akaniuliza, hawezi nini paa? Hamwambia, maongo yote yameuma, hana pahali pamoja pasipomwuma. Akaniambia bwana, Katwae ule mtama wa felefele, mfanye uji mpe. Bibi akanena, Eh! bwana, paa ndio mboni yako wa macho, wewe huna mtoto, humfanya paa kama mwanao, wewe huna karani, humfanya paa ndio kama karani wako, wewe huwezi kusimamia, humfanya paa kama msimamizi wako, bassi bwana kumi kwako hatta moja halipatikani lilio jema kwako, paa huyu, bwana, si wa kutendwa mabaya, huyu ni paa umbo, si paa kwa moyo, moyo wake na mambo yake ampita mngwana, alio yee yote, bora.

Akamwambia, Wewe mpuzi, maneno yako mengi, thamani yake mimi namjua yule, nimemnunua kwa thamani ya themuni, bassi mimi nina hasara gani?

Akamwambia, Bwana sitazame hayo yaliopita, tazama haya yalio usoni pako. Huyu si paa wa thamani ya themuni, wala lakki, huyu neno lake na tasfida yake anapotuliza ulimi wake kunena na akili yake, yapita lakki mbili.

Eh! maneno yako mengi, mwanamke saa, hupunguzi?

Yule mzee akamjibu paa, Nikaambiwa na bwana, utwaliwe mtama wa felefele, ufanywe uji unywe.