Page:Swahili tales.djvu/142

This page has been proofread.
122
SULTANI DARAI.

kwa bwana wake, anamwonea huruma, taabu yaliompata huyu paa, ndio mambo ya ulimwengu.

Yule mkewe Sultani, aliposikia maneno yale mumewe kumwambia mzee, akapotewa na nuru za uso, akaingiwa na imani roho yake, akatoka na machozi katika macho yake, hatta mumewe, alipomwona anatoka na machozi, na nuru za uso zimempotea, akamwuliza, una nini, binti Sultani? Akamwambia, katika ulimwengu asio mengi ana machache, na mtu wazimu wake ndio akili yake.

Kwa nini, bibi, ukanena maneno haya?

Akamwambia, nakusikitikia wewe, mume wangu, kwa haya unayomtenda paa, killa ninapokwambia neno jema kwa paa, mume wangu, hutaki wewe na akili yako tu. Nakuona huruma mume wangu, akili yako kukupoteza.

Akamwambia, Kwani ukanambia neno hilo?

Akamwambia, Shauri mbaraka tu, watu wawili katika nyumba, mke na mume, mke akipata neno, amwambie mume, na mume akipata neno, amwambie mke, kwani shauri mbaraka.

Akamwambia, mwanamke wewe una wazimu, tena wazimu wako u thahiri, tena wataka kutiwa pingu.

Akamwambia, Bwana, mimi sina wazimu, kana mimi nna wazimu, huu wazimu wangu ndio akili yangu.

Akamwambia, Ee kizee, usisikilize maneno ya huyu bibi, ukamwambie, potelea mbali. Kamwambia paa, asinifanye uthia, tena asikae huko chini akajifanye yeye ndio Sultani, mimi huku sipati usingizi wa usiku, wala wa mchana, sipati kula, wala sipati maji ya kunywa, kwa uthi wa yule paa anaokuja akiniuthi. Marra