Page:Swahili tales.djvu/152

This page has been proofread.
132
SULTANI DARAI.

kwa shari, hatta paa amekufa kwa ghathabu na uchungu katika nafsi yake, tena umeamru watu wakamtupa ndani ya kisima! Ah! twache tulie.

Akachukuliwa paa akatupwa ndani ya kisima kilichotekwa maji.

Yule bibi aliposikia darini, akaandika barua mbiombio, upesi upesi, harraka harraka, akamwambia, Baba yangu nimekuletea barua hiyo ukiisha kuisoma, ingia njiani uje. Akaiba punda watatu, akawapa watumwa watatu, akawaambia, pandeni, mwenende mbiombio na punda, hatta mkipa baba yangu barua, akiisha isoma, mwambieni upesiupesi twenende. Na wewe nimekuacha huru, na wewe wa pili nimekuacha huru, na wewe wa tatu nimekuacha huru, kwa sababu ya barua hii mwipeleke upesi.

Watu wale wakaenda mbiombio na punda, usiku na mchana, hatta wakafika, wakampa barua Sultani. Alipoisoma barua hili Sultani akanama, akalia sana, kama mtu aliofiwa na mamaye, akaona huzuni sana Sultani. Akaamuru Sultani kutandikwa frasi. Akaenda akaitwa liwali, akaenda wakaitwa makathi, wakaitwa na jamii matajiri, waliomo katika mji. Akawaambia, haya, nifuateni upesi, tumefiwa, twendeni tukazike.

Akatoka Sultani, akaenda usiku na mchana, hatta akawasili pale kisimani, alipotupwa yule paa.

Akaingia mwenyewe, binafsi yake Sultani, ndani ya kisimani, akaingia na waziri binafsi yake, wakaingia makathi binafsi yake, kisimani, wakaingia na matajiri makuu ndani ya kisima, wakamfuata Sultani. Sultani alipomwona paa ndani ya kisiwa, alilia sana, na wale