Page:Swahili tales.djvu/172

This page has been proofread.
152
MOHAMMADI MTEPETEVU.

labuda katika inchi ya Bássara kuna mtu mmoja kijana jina lake Mohammadi mtepetevu, huko itapatikana.

Kalifa akamuita waziri wake Masruri Sayafi. Akamwambia, twaa khati, usafiri wenende Bássara kwa liwali Mohammad Zabidi. Naye ndiye liwali wake, kalifa, alioko inchi ya Bássara.

Akapewa khati Masruri Sayafi, akafuatana na jeshi ilio nyingi, wakasafiri kwa njia barra, wakaenenda hatta il Bássara. Wakaingia katika inchi ya il Bássara, wakafikilia kwa liwali Mohammad Zabidi.

Akatoa khati akampa, akasoma. Alipokwisha soma, akamkaribisha nyumbani, akamfanyizia karamu ilio kubwa, wakaingia wakala chakula. Walipokwisha, akamwambia, Sina amri mimi ya kukaa kwako. Amri yangu niliopewa ya kukupa khati, ukiisha soma, twenende kwa Mohammad mtepetevu. Na sasa toka twenende. Wakatoka wakafuatana, wakaenda kwa Mohammad mtepetevu.

Waziri Masruri Sayafi akatoa khati itokayo kwa Harun Rashidi. Akapokea kwa mikono miwili, akafungua kwa adabu, akaisoma khati itokayo kwa kalifa.

Alipokwisha soma, akamwambia, Karibu nyumbani. Akamwambia, sina amri mimi ya kuingia nyumbani mwako, nimeambiwa nikupe khati, ukiisha soma tufanye safari, twenende. Kwani kalifa ameniambia, usikae, mpe khati uje zenu, mfuatane naye yule. Alipoambiwa vile akanena, sema'a wa ta'a, lakini tafáthali unywe kikombe cha kahawa. Akamwambia, sikuamriwa mimi kunywa kahawa kwako. Akamwambia, huna buddi kunywa kahawa