Page:Swahili tales.djvu/174

This page has been proofread.
154
MOHAMMADI MTEPETEVU.

yangu. Akamnasihi, akakubali kwa nguvu, akaingia ndani ya nyumba, akapanda darini katika sébule yake. Akamkaribisha, akaingia ndani, akakaa kitako.

Alipokaa kitako akaletewa mfuko wa dinari khamsi mia. Akamwambia, tafáthali uingie katika hamami, kwani siku nyingi umetaabika kwa safari mwendo wa barra, huna buddi na kuchoka. Bassi tafáthali uingie katika hamami.

Bassi akaondoka akaingia katika hamami, na maji yake, yalio katika hamami, marashi mawáridi, ndio maji yake yaliomo. Akaingia akaoga. Wakaja na vitwana matowashi, wakaja, wakamsugua kwa vitambaa vya hariri. Alipokwisha, akatoka, akapewa nguo za kukaukia maji, na killa nguo ni nguo hariri na zari. Akakaukia maji. Alipozivua, akaletewa baksha ya nguo nyingine, nguo zayidi ya zile za kukaukia maji. Akavaa, na zile zikakunjwa, zikawekwa na ule mfuko aliopewa kwanza. Akaenda zake sebuleni akakaa kitako.

Alipokaa, akainua macho akatezama sebule, pambo lake, na matandiko yake yaliotandikwa chini. Akaona ajabu kuu, akawaza moyoni mwake, hatta chumba cha kalifa hakikupambwa kama hivi. Akaletewa maji, akanawa, yeye Masruri Sayafi, na liwali, Mohammad Zabidi, na waliopo sebuleni wote. Walipokwisha nawa wakaona vitwana wakaingia na vyakula, wakaja wakaandika, wakala. Walipokwisha kula, akawaza, vyakula vile ni vyakula ambavyo havimo katika ulimwengu.

Akapewa chumba cha kulala, Akaingia chumbani mwake, alichofanyiziwa kulala, wakaja vijakazi, wamevaa