Page:Swahili tales.djvu/176

This page has been proofread.
156
MOHAMMADI MTEPETEVU.

lebasi njema njema, killa mmoja na kinanda, wakaingia wakapiga kinanda, wakaimba, ili kumtumbuiza, na wangine kucheza, na kutoa mashairi ya kumsifu. Akapata usingizi akalala usingizi wa mchana.

Alipoamka watu wamekaa tayari mlangoni, kumngoja kwenda naye katika hamami. Akaenda katika hamami, akavua nguo, zikakunjwa zikawekwa pamoja na zile za kwanza. Akaingia katika hamami, na hali ile ile ya kwanza na ziyada. Bassi alipotoka katika hamami, akapewa nguo za kukaukia maji. Alipokwisha kukaukia maji, akavua na nguo hizi za hariri na zari. Akaletewa nguo nyingine ya kutokea sebuleni, na killa nguo methmini. Akavaa, akatokea nje.

Akitoka, chakula tayari, wakaingia, wakala chakula. Wakaisha wakajizumgumza hatta usiku ukaingia, akatandikiwa chumba kingine. Akaenda kulala. Akitezama chumba chile, pambo lake liliomo, na samani zake, chapita chumba alicholala mchana. Akalala hatta assubui.

Akaamka, wakaja watu wakamtwaa, wakaenda naye katika hamami. Akitoka akapewa nguo nyingine za kukaukia maji, akaisha akaletewa nguo nyingine, akavaa. Na zile alizovaa kwanza zikakunjwa, zikawekwa, na killa anapoletewa nguo, huletewa na mfuko wa dinari khamsi mia.

Akatoka nje akaenda akala chakula. Walipokwisha kula, akamwambia Mohammad mtepetevu, Mimi sina ithini ya kukaa siku mbili, na leo siku ya pili hii, bassi fanya safari twende zetu.