Page:Swahili tales.djvu/182

This page has been proofread.
162
MOHAMMADI MTEPETEVU.

anakwenda katika inchi ya Sini. Bassi twaa dirhamu tano hizi umpelekee, labuda huko aendako, atakununulia bithaa, uje upate fayida hapa, kwani Sheikh ni mtu mmoja mtaowa, apenda maskini, bassi ondoka ukampelekee hizi dirhamu tano. Nikamjibu, mamangu, kwenda siwezi, wala usiniambie tena maneno haya. Akaniambia, kana hutaki kwenda, bassi nami nitakutupa, sikupi chakula, wala sikupi maji. Wala ukilala juani, sikuondoi, nitakuacha kufa njaa yako. Akaniapia na kiapo. Nikaona tena utakufa mimi.

Nikamwambia kama huna buddi, nisogezee vyatu vyangu. Akanisogezea, nikamwambia, nivike miguuni, akanivika. Nikamwambia, nipe na kanzu yangu, akaniletea. Nikamwambia, nivike. Akanipa na nguo ya kujitanda. Nikamwambia nipe na gongo langu mkongojo, nipate kujigongojea. Akanisogezea. Nikamwambia, niondoe bassi, nisimame, akaniondoa. Nikamwambia, kaa kwa nyuma ukanisukuma, nipate kwenenda. Bassi ikawa hali hiyo, akinisukuma, hiinua mguu moja, hatta tukafika pwani. Tukamtafuta Sheikh Abalmathfár. Yu katika kupakia.

Aliponiona akastaajabu, akaniambia, Vilikuwaje leo, hatta ukafika pwani huku? Nikampa dirhamu zangu tano zile, nikamwambia, amana yangu hii, nichukulie huko wendako, uninunulie bithaa, ndilo jambo nililokujia pwani. Akazipokea Sheikh Abalmathfár.