Page:Swahili tales.djvu/188

This page has been proofread.
168
MOHAMMADI MTEPETEVU.

nivika viatu vyangu na nguo zangu. Bassi nikamwambia, nipe fimbo yangu, akanipa fimbo yangu. Nikamwambia, kaa nyuma ukanisukume. Akakaa nyuma akanisukuma, nikainua mguu moja, akanisukuma, nikainua mguu moja, hatta tukafika.

Nikaonana naye nikampa mkono. Akaniuliza hali, akaisha akaniambia, amana yako itakuwasilia nyumbani. Tulipokwisha onana, tukatoka, na mama yangu akanisukuma, hatta nikafika nyumbani kwetu. Nikafika, nikarejea mahali pangu, nikalala.

Kitambo kidogo nikaona mtu akaingia, akaja akinipa kima. Yule akaniambia, Salaam Sheikh Abalmathfár. Nikapokea kima yule, nikamwacha, akatokea yule mtu alioleta kima.

Nikamwita mama yangu, akaja, nikamwonyesha, nikamwambia, kitu kikubwa alichoniletea Sheikh Abalmathfár, hapa petu kima wanakuzwa kumi kwa dirhamu, na dirhamu tano ameniletea kima moja.

Sijadiriki kwisha kusema maneno haya na mama yangu, nikamsikia mtu, akibisha—Hodi! Nikamwambia? karibu. Akaingia na funguo, akanipa funguo zile. Naona na mahamali nyuma yake, wakaingia wanachukua makasha makubwa mno ajabu. Akaniambia, hizi funguo za makasha haya. Nikamwuliza, makasha haya ya nini kuniletea mimi? Akaniambia, hii ndio amana yako uliompa kwenda kukununulia bithaa.

Nikamwambia, hana haja Sheikh Abalmathfár ya kunithihaki, mimi maskini ya Muungu. Mimi kijana mbele zake, na yeye mtu mzima mbele yangu. Hana haja