Page:Swahili tales.djvu/200

This page has been proofread.
180
MOHAMMADI MTEPETEVU.

Bassi wamemwambia, mchukua bwana wako huyu, wende naye hatta mji wa Nuhás, aliko mkewe. Akamwambia, nasikia. Bassi wakamwambia, inama, akainama, wakanitwaa wakanipandisha juu yake. Akaniambia, huyu ni Maridi, bassi hapo ulipo juu yake usithukuru ismu ya Mwenyi ezi Muungu, kwani ukithukuru ismu ya Mwenyi ezi Muungu atayeyuka huyu, kwani huyu ni Maridi. Nikawaambia, sitathukuru.

Akaniambia, jizuia sana juu yangu. Nikajizuia sána. Alipokwisha nizuia, akaruka, akaenda juu, nami nili hali ya kuwa juu yake. Akapaa hatta tangu ulimwengu nilipokuwa, inchi nikiona hatta nisione tena, nikaliona hewa tu. Hatta tukaenda, tukasikia tusbiih za Malaika katika mbingu, naye alina na ghathabu ya kupaa.

Bassi katika kupaa kule, nikamwona mtu kijana, sura njema sana, amepiga na kilemba cha shali akhthár, amechukua na kimwondo cha moto. Akaniita kwa jina langu, Mohammadi mtepetevu! Aliponiita, nikamwitikia. Akaniambia, thukuru ismu ya Mwenyi ezi Muungu, ao usipothukuru nitakupiga kimwondo. Nikathukuru.

Kadiri ya kuthukuru, jini aliniacha, nalitoka juu ya maongo yake. Marra kijana aliponiacha, akampiga kile kimwondo alichochukua mkononi, akayeyuka kama rissás.

Bassi nikawa kujijia zangu hatta nikafika chini. Nikaanguka katika habari. Kuangukani kwangu nikaona chombo cha wavuvi. Waliponiona, wakaja wakaniokota, wakanipakia katika chombo chao. Wakanitolea samaki, wakaniokea, nikala. Nilipokwisha kula nikaona sijambo punde. Ikawa kusema nami, na ile lugha yao hatusikizani.