Page:Swahili tales.djvu/206

This page has been proofread.
186
MOHAMMADI MTEPETEVU.

mwuliza, aliyekuleta huku nani? Akaniambia, alionileta huku ni yule nyani. Ulipokwisha kufanyiza amali ile, naliona mtu akanichukua, bassi hatukukaa mahali illa huku. Na killa mahali atakapo kukaa, hapakumweka, illa huku, kwani huku mwana Adamu hana tamaa ya kufika huku. Bassi sasa amekuja aniweke huku. Naye amekwenda tembea, bassi huku haji isipokuwa kwa siku zake. Na sasa usifanye khofu wewe, maadám ya kufika huku wewe tukaonana mimi nawe, na kwetu tutakwenda.

Bassi akanieleza khabari zake. Akaniambia, amri zote za Majini ya katika mji huu wa Nuhás, amri zake, zina yeye. Naye ana amali hufanyiza za kuwafunga Majini. Nawe sasa enenda. Akaniagiza. Utaona mtaimbo, una na pete, pana na chetezo, pana na buhuri. Utwae buhuri, utie ndani ya chetezo, ufukize mtaimbo, usome na azma zake, utwae pete hii, ugonge na mtaimbo ile pete, iliomo na mtaimbo. Bassi watakutokea Majini, kulla namna, kulla mmoja kwa fazaa ya nafsi yake. Na watakapokuja, watakuambia, sisi tu watumwa wako, na amri amri yako, tuamru utakalo, tutafanyizia. Bassi wakiisha kuja, amri ni ya wewe, lile utakalo kumtenda nathari yako tena.

Na maneno haya mke wangu amenieleza. Nikaondoka, nikaenda upesi palipo mtaimbo, nikatenda kama alivyoniambia. Nalipokwisha kwa kugonga mtaimbo ule, marra naona waana wanitokea, wangine jicho moja, wangine mkono moja, wangine mguu moja, kwa kulla namna wakanitokea. Wakaniambia, neno gani utakalo, sisi watumwa wako, na amri ni wako. Nena utakalo. Nikawaambia mimi, yuko wapi Maridi aliokuja na mke huku, ndiye aliogeuzwa nyani? Wakaniambia, hako amekwenda