Page:Swahili tales.djvu/208

This page has been proofread.
188
MOHAMMADI MTEPETEVU.

tembea, lakini mwezi wa pili ametoka kuenda kutembea, na huu ndio wakti wake wa kuja. Nikawaambia, upesi mfungeni, mleteni. Marra ile nikamwona ameletwa mbele yangu, naye mikono nyuma. Nikamwuliza, wewe ndiye uliomchukua binti yule? Akaniambia, ni mimi. Bassi nikamwambia, kama Sherifu aliokugeuza nyani akakutupia ulimwenguni, mimi nitakutia ndani ya chupa la shaba nitakutupa baharini.

Bassi nikamtwaa yule, nikamtia ndani ya chupa la shaba. Nikamchukua kwa binti yule, tukamtupa baharini. Bassi nikawaamrisha Majini, killa kitu cha tunu, cha hedaya, kuvichukua. Na mimi na mke wangu tumekaa juu ya ulili, na mtaimbo, na chetezo, na buhuri yake, na kulla kinipendezacho. Nikawaamrisha Majini kutuchukua.

Wakatuchukua Majini hatta tukafika mji wa Bássara, wakanitia ndani ya nyumba yangu. Nikamwita mkwe wangu, Sherifu, assubui, akaja na mama yangu na jamaa zangu, na nipendao. Wakaja, tukaonana kwa furaha, kwa kusema, na kwa kucheka. Ikafanya harrusi vingine tena, tukafanya harrusi kubwa na furaha, na babaye binti yule akafuraha mno. Bass, tukakaa kitako kwa furaha, kwa kusema na kucheka.

Na haya, usinene mimi kukufanyizia kwa sababu ya kuogopa, lakini nimeona vitu hivi havinisulihi mimi, bassi nimeona ni kheri nikupe wewe, wewe Kalifa mtu mkubwa, na mimi mtu mdogo.

Kalifa akamwambia, ahsanta, nawe kaa kitako papa hapo, usiende tena Bássara. Wakatolewa watu kwenda Bássara, kwenda kuhamisha vyombo vyake. Wakaja navyo inchi ya Baghdadi, akakaa kitako raha mustarehe.