Page:Swahili tales.djvu/220

This page has been proofread.
200
SULTANI MAJINUNI.

Amenena naye sana, hasikii, amempiga, hasikii, amemfunga, hasikii, bassi tena Sultani amechoka mambo yake, amemwachilia mbali.

Akakaa Sultani, hatta ule mtende wake, kikachanua kilele, hatta baada ya mwezi kupita, akapata dalili ya kuzaa mtende wa Sultani, akafurahi sana, akamwita waziri, akamwambia waziri, mtende wangu unazaa. Akamwambia amiri, mtende wangu unazaa. Akawaambia makathi, mtende wangu unazaa. Akawaambia na wote matajiri wangwana waliomo katika mji.

Akakaa baada za siku kupita, mtende zile tende zinafanya kuiva. Akawaita watoto wake wote sita. Akawaambia, yule mtoto mmoja hamo pamoja nanyi, amekaa kamma mwanamke, bassi nipeni shauri yenu waanangu. Wakamwuliza, kama ipi, baba? Akawaambia, nataka mtoto mmoja katika ninyi akaungojee ule mtende hatta tende ziwive, nipate kula tende zile. Siwezi kuwacha mtende ule pekeyake, naogopa watumwa watakula, ao huja ndege wakala. Bassi nataka wende ukaungojee mtende. Akamwambia, Ee walla! Akaenda zake.

Kumejengwa nyumba njema. Akikaa kitako kule hatta usiku. Akawakusanya watumwa wote wa shamba, wakapiga ngoma chini ya mtende. Aogopa yule kijana, akasema, nikilala ndani, huenda mtumwa akaja usiku akapanda juu ya mtende, akaiba tende, ao huenda akaja ndege mkubwa usiku akala tende, na tende zimewiva tena. Bassi na tucheze ngoma hapa chini ya mtende hatta ussubui.

Wakapiga ngoma, hatta ulipokoma nussu ya usiku waka-