Page:Swahili tales.djvu/232

This page has been proofread.
212
SULTANI MAJINUNI.

kuzaa kupona, kumbe kuzaa kwangu mimi ni kufa? Vijana viwili mwaliokwenda katika bustani, pasiwe mtoto alionilimbusha tende. Bassi kuzaa huku kwa nini na watu wanena, mwenyi kuzaa kupona, na kupona huko? Msinene, ninyi watoto, mtanitia mimi roho, kupona kwangu ni kutaka kitu nikakipata, roho yangu ikafurahi, ndio kupona kwangu ni kumwona mtu ataka kunipiga, ukapigana naye ukanigombea mimi baba yako, ndio kupona kwangu, nikikutuma pahali, ukaenda, ukajua kunena na watu, ukajua mazumgumzo na watu, ukamjua mkubwa na mdogo, ukamjua tajiri na maskini, bassi ndiko kupona kwangu. Bassi, nyie waanangu, mwaka wa pili huu sipati kula tende, tende zangu mimi, huzisikia kwa mashikio, kwa macho nisizione. Bassi niondokee enenda zako. Akaondoka akaenda zake.

Akawaambia, ninyi, waanangu waliosalia watu wanne. Ukizaa sasa mtende, atakaokwenda akaungojea hatta nikapata tende nikazilimbuka, nitamfanyia harrusi ya miezi mitatu.

Killa mtu pale wale vijana wananena, baba, nitakwenda mimi; na mwingine, baba, nitakwenda mimi; na mwingine akamwambia, baba, nitakwenda mimi; na mwingine akamwambia, baba, nitakwenda mimi. Akawaambia, vema, killa atakaye na aende, lakini mimi nataka waenende mmoja mmoja. Wakamwambia, Vema, bwana.

Akakaa muda wa miezi mingi ukazaa mtende, ukazaa sana, ukaacha kuzaa, ukawayawaya. Akawaambia watoto, mtende umezaa, na mwaka huu kuzaa kwake ni sana kuliko miaka yote. Akamwambia, nitakwenda mimi baba, yule mkubwa kuliko hawa. Akamwambia, ngoja kwanza zipevuke. Bassi akakaa kitako hatta akaletewa khabari,