Page:Swahili tales.djvu/238

This page has been proofread.
218
SULTANI MAJINUNI.

na harrusi miezi minne. Wakamwambia, vema baba, utakula tende mwaka huu.

Wakakaa hatta siku kumi zalipopita tende zimekuwa pevu, akaja akaambiwa, kama tende zimekuwa pevu. Akamwambia, vema, utakapoziona moja moja zinawiva, njoo nambie. Akakaa hatta muda wa siku tano, akaja yule nokoa, akaja kumwambia bwana, tende zinawiva na mapooza yanaanguka. Akakaa muda wa siku tatu, akamwambia, enende.

Akaondoka kijana kwa furaha kwa nguvu, akaenda hatta akawasili katika bustani. Akamwambia, mimi sitalala, nitapanda frasi nizunguke leo usiku kucha humo. Akatwaa bunduki yake, na baruti yake, na marisao yake, na fataki zake. Akapanda juu ya frasi, akizunguka katika bustani. Akazunguka sana hatta yalipokoma saa saba ya usiku, akasikia kaanga analia nyuma ya bustani, akanena sasa kumekuwa saa saba u nussu, nitatoka nimfuate huyu kaanga, anayolia katika bustani. Akitoka akamfuata yule kaanga kule anakolia, naye kaanga yuko mbali; lakini ule usiku anamsikia yuko karibu. Akaenda hatta nuss ya njia, ndege nyuma amekuja mtendeni akila tende, asisaze hatta moja, naye kule hajarudi, naye kule kaanga asimpate, akarudi akija zake.

Hatta alipofika katika bustani akitupa macho juu, tende hamna. Akashuka juu ya frasi, akakaa chini ya mtende, akalia sana. Hatta wakaja watumwa wake. Je! Bwana, unalilia nini? Akawaambia, mimi silii kwa kuogopa baba, nalia kwa kukosa tunu aliotaka kunitunikia baba.