Page:Swahili tales.djvu/240

This page has been proofread.
220
SULTANI MAJINUNI.

Akamwambia, tunu gani inavyokuliza mno hivi? Akawaambia, baba ameniambia atanioza mke mzuri, atanifanya na harrusi miezi minne, naye ameniambia atajua kama mimi ndiye mwanawe, sasa zote tatu sikupata hatta moja, bassi mimi nina buddi na kulia kwa kuyakosa haya? Bassi tena nitakwenda zangu, nitamjibu.

Hatta alasiri akaenda kwa babaye, amwambia, Baba, masalkheiri! Babaye asimwitikie. Akanyamaa. Akamwambia, zi wapi tende? Akamwambia, tende, baba? tende zimekwisha liwa na ndege. Akamwambia, enende kamwambia mama yako ndani akupe dusamali, uvae, akupe na barakoa, uvae, akupe na kanzu, na suruali uvae, akupe na shela ya kujitanda, akiisha, atafute mume akuoze. Niondokelee mbele ya uso, sipendi kukuona.

Akaondoka mkewe, akamwambia, vijana hawa hawaendei kutazama huu mtende, kwenda kucheza na kulala. Wallakini tufanyeje? Na tungoje hatta safari hii tena uzaapo.

Akakaa Sultani muda miezi mingi kupita. Mtende ukazaa; akaletewa khabari shamba na nokoa wake, Bwana, mtende umezaa. Umezaa kama mwaka jana, ao mwaka huu zayidi? Amwambia, Bwana, kitu kikiwa kidogo, mtu hakitumaini, kama mtu anakitumaini kitu kilicho kidogo ningekwambia bwana, mtende huu ni nyingi kuliko miaka yote, wallakini ni kitu cha kupukutika, lakini na tutazame hatta zitakapopea. Amwambia, vema, ukiziona zinapokwanza kuanguka na mapooza, njoo nambie. Akamwambia, Inshallah, bwana.