Page:Swahili tales.djvu/242

This page has been proofread.
222
SULTANI MAJINUNI.

Sultani yule ana paka, ampenda sana, na paka mzuri sana, na yule paka mkuza sana, paka yule mwanzo wake aliyekikamata kuku vidogo vitoto. Akaambiwa Sultani, paka anakamata kuku, akawaambia, paka wangu na kuku wangu, bassi mwacheni.

Tende zile zikawiva shamba, akaletewa khabari na nokoa wake, akamwambia, bwana, tende zinawiva sana, nathani zikikawia hatta kesho zitaharibika kwa sababu zilioiva; na mwaka huu hazikuanguka mapooza mengi, ni kutwa ni nane tissia, kwa ginsi ya mtende kupevuka sana. Bassi nilete mtoto atakuja kuungojea mtende. Sultani akawaambia wale wawili waliobaki, akawaambia, leo enendeni nyote wawili mwaliosalia. Wakamwambia, Ee walla, baba. Wakajifunga, wakaenenda hatta wakifika katika bustani.

Wakawaambia wale watumwa walio shamba. Wakawaambia, tumekuja sisi simba, tumekuja mtazama huyu ndege anayokuja akila tende hizi, bassi leo ajali yake imekwisha, na ajali yake ni katika mkono wetu. Wakawaambia, hapa sisi labuda bunduki isiwake moto. Wakawaambia, vema, bwana. Wakakaa kitako hatta usiku. Wakawaambia, kokeni mabiwi ya moto katika bustani. Wakakoka mabiwi ya moto. Ukawaka moto sana katika bustani mle, itakapoanguka sindano utaiona kwa sababu wanga wa moto. Wakakaa hatta saa ya saba ikipiga, likatanda wingu kuu la mvua, na tufani ikawa nyingi, hatta yalipokoma saa ya nane u nussu ikanya mvua sana, na baridi nyingi, na kiza kikawa kipevu, alipo hapa hamwoni aliyo hapa, labuda wasikilizana sauti, na kumwendea mwenziwe kumpapasa, ndipo atakapomjua