Page:Swahili tales.djvu/246

This page has been proofread.
226
SULTANI MAJINUNI.

Akitoka nje nokoa, wakaamkiana. Je! nipe habari ya mjini. Akamwambia, habari ya mjini njema, nimetumwa kuwatazama watoto, hatta sasa hakupata khabari zao, wazima wamekufa, wagonjwa, tende Sultani atapata alimbuke, ao hapati, bass. Akamwambia, twende nikupeleke waliko watoto. Akaenda, akawakuta wakakaa maongoni wote wawili, wamejikunyata wanatetemeka kwa baridi yalivyowashika.

Wakamwambia, Je! Hweduni! habari za mjini? Akawaambia njema, akina bwana, baba yenu salaam, baada ya salaam amwona kimya hatta sasa, jua limekuwa saa ya nne. Ah! kweli? Akawaambia, kweli saa ya nne, bwana. Wakamwambia, siye tunanena labuda sasa ufajiri? Akawaambia, hakuna bwana, mimi nimeondoka mjini saa ya pili, nalipotumwa huku shamba. Bassi yee, akina bwana, Bwana anauliza, atakula tende mwaka huu, ao hali? Akaondoka yule mmoja, umwambie atakula mwaka huu tende, pana mwaka huu, pana sasa hivi. Ngoja nikukatie, nikupe ukampelekee.

Yule nduguye akamwambia, wewe unasema kwa akili yako, ao una wazimu? Akamwambia, kwa nini? Akamwambia, nakuuliza kama umenena kwa akili yako, nipate kujua kujibu. Akamwambia nanena kwa akili yangu, wala sina wazimu. Akamwambia, wewe una wazimu khálisi, tena wazimu wako wa kutiwa pingu, na mti kati, na mnyoo, ndipo ufanywe dawa upone. Akamwambia, kama wewe huna wazimu, hungenena maneno kama hayo, kwenda kumwambia baba. Akamwambia, kwa nini?