Page:Swahili tales.djvu/248

This page has been proofread.
228
SULTANI MAJINUNI.

Hapa killa siku, na killa mwaka, unangojewa mtende, na ndugu zetu wasilale hatta marra moja, na wakapotewa na usingizi. Marra moja akizindukana tende zimeliwa. Bassi sisi walioondoka tokea saa saba mtendeni, tukaja zetu hapa tukalala hatta sasa saa ya 'nne, tende hizi zitungoje sisi? Killa siku watu hulala chini ya mtende, na ndege huja akala tende akaenda zake. Eh! sisi tumelala huku nyumbani, ndege huyu atangojea sisi?

Ah! Labuda báhati yetu kwa mvua ile, na giza lile, na tufani ile, labuda yule ndege hakuja. Akamwambia, bassi mvua zile, na giza lile, na tufani ile haimkatazi ndege kuja kula tende. Bassi, mimi ninakwenda tazama. Enenda wewe ukatazame, mimi siendi pahali, najua tende hakuna. Niende yani kusumbuka burre, nikapate mvua, nipate na baridi, nipate na umande wa burre, nami najua tende hakuna katika mtende, zimeliwa na ndege zote. Lakini yule anaokwenda mpumbavu, ataka kudanganya roho yake, kama hamsadiki, na ngojeni hatta atakaporudi.

Yule akaenda, hatta katika mtende, akaona hamna tende hatta moja, hatta mapooza yalioanguka chini hapana. Akarudi hatta akafika kwa nduguye. Je! tende ziko? Akamwambia, Ee bwana wee, mwenyi kuuona mtende, akiambiwa mtende huu mwaka huu ulizaa, tena jana yalikuwamo tende, hasadiki, gissi ya mtende walipo kuharibika, hatta dalili ya kuambiwa mtende huu umezaa hapana.

Akamwambia, mimi sikukwambia papa hapa, kama hakuna kitu? Sasa nipe shauri, pana shauri sasa? Na twende kwa baba yetu, tukaenda tukamwambia, tende