Page:Swahili tales.djvu/254

This page has been proofread.
234
SULTANI MAJINUNI.

utafaa nawe moja? Roho yangu imefanya khofu, sababu ya mtende, nasikia umezaa sana, na tende nzuri, bassi naogopa kukupeleka kuzikosa tende kuzila. Akamwambia, na leo stahamili, nache niende baba, utazame nami bahti yangu, utakula tende, ao utazikosa.

Mkewe akamwambia, Bwana, mwache aende mtoto, tujaribu, huenda tukapata tukala tende, ao tutakosa, bassi mwache aende mtoto. Akamwambia, mke wangu, miye sikatai kwenda mtoto, roho yangu hayamini. Akamwambia, haithuru bwana, mwache aende mtoto. Akamwambia, baba, kesho tukiwa wazima mimi, nawe, na mama, kesho utakula tende baba. Akamwambia, na nduguzo walinena vivi hivi, kama baba utakula tende, nami sili. Akamwambia, haya enenda zako shamba.

Hatta alipofika katika bustani, Akawaambia watumwa wote wa shamba, laleni. Wakamwambia, Ah! bwana tutakuacha pekeyako? Akawaambia, usiku haunili kama ntauogopa. Wakamwambia, bass, bwana, kua heri. Akawaambia, kua herini.

Na yule kijana akaingia ndani akalala, akalala sana hatta saa ya saba ikipiga, akiondoka akija hatta mtendeni. Akakaa kitako akitafuna bisi, na zile bisi ndani zina changarawi; hutafuna zile bisi, akitaka kusinzia, hutafuna ile changarawi, akiamka, ikawa kazi hiyohiyo, hatta yule ndege akija, naye amemwona.

Yule ndege alinena, hapana mtu, kwani yeye alikaa mbali na mtende. Hatta alipotua palipo mtende, yule kijana akaondoka, alipotaka kunyosha mdomo kula tende, amemshika bawa.

Ndege kuondoka kwake panapo mtende aliruka,