Page:Swahili tales.djvu/262

This page has been proofread.
242
SULTANI MAJINUNI.

wakachukuliwa. Je! nokoa tupe khabari waliotutia. Akawaambia, naliokutiani? Wakamwambia, twambia nokoa wetu. Akawaambia, bwana hakuzaa mwana, amezaa simba. Akawaambia, katazameni mkaa jikoni, alivyofunua uso wake leo kwa baba yake. Gissi gani, nokoa? Akawaambia, leo siku ya watu kula tende. Kweli, nokoa? Akawaambia, na'am.

Akawaambia, kwanza msiende kumwamsha illa twende tukampukuse, mwenyi kuku na achukue kuku, na mwenyi mbuzi na achukue mbuzi, na mwenyi mchele achukue mchele, na mwenyi mpunga na achukue mpunga, na mwenyi ngano achukue ngano, na mwenyi fetha achukue fetha; lakini mtama, na muhindi msichukue haya.

Watu wakaenda majumbani mwao, wakaja, aliochukua kuku amechukua, aliochukua mbuzi amechukua, aliochukua mchele amechukua, aliochukua mpunga amechukua, aliochukua ngano amechukua, aliochukua fetha amechukua. Wakachukua na ngoma, wakamkuta amelala chini ya mtende.

Wakaenda pale wakamchukua kwa baragumu, kwa zomari, kwa ngoma, na kofi, na vigelegele hatta kwa babaye.

Babaye aliposikia shindo linakuja njiani, na matawi la mtende limechukuliwa ndani ya pakacha, alipoona watumwa wa shamba wanakuja kwa furaha, alipomwona na mtoto amechukuliwa juu kwa juu, Sultani Majnuni alijua, leo nitakula tende. Akamwita, mke wangu! Akamwitika, lebeka, bwana. Akamwambia, bwana wa jiko leo atatuli-