Page:Swahili tales.djvu/268

This page has been proofread.
248
SULTANI MAJINUNI.

Akakaa baada ya siku ya pili, akakamata punda. Akaenda akaambiwa, Sultani, paka amekamata punda, akawaambia, punda wangu na paka wangu. Akakaa baada ya siku moja, akakamata frasi. Akaenda akaambiwa Sultani, bwana, paka amekamata frasi. Akawaambia, paka wangu na frasi wangu. Akakaa akajikamatia ngamia. Akaambiwa Sultani, paka leo amekamata ngamia. Akawaambia, wamtakia nini, paka wangu na ngamia wangu, ninyi paka huyu hampendi mwataka ni'mue, killa siku kuniletea maneno maneno tu. Nami si'mui mwacheni ale ngamia, hatta mtu na ale.

Akakaa hatta siku ya pili, akakamata mtoto wa mtu. Akaenda akaambiwa Sultani paka amekamata mtoto wa mtu. Akawaambia paka wangu na mtoto wangu. Akakaa siku ya pili akakamata mtu mzima, akaenda akaambiwa, amekamata mtu paka, bwana. Akawaambia, paka wangu na mtu wangu.

Akahama mjini yule paka, akakaa kama katika Mnazimoja katika magugu. Bassi akipita mtu hwenda maji, humla, akiona ng'ombe akipita kwenda kuchungwa, akamkamata akala. Akiona mbuzi akamata, akila. Kitu akionacho cho chote kinachopita katika njia ile, akamata akila.

Watu wakaenda wakamwambia Sultani, Gissi gani Bwana, wewe ndio Sultani wetu, wewe ndio bwana wetu, wewe ndio ngao yetu, umemwacha yule paka bwana, amekwenda kaa Mnazimoja, akipita mtu humla, akipita ng'ombe humla, akipita punda humla akipita mbuzi humla, cho chote kitu kinachopita katika njia ya Mnazimoja hukamata akila, na usiku hushukia katika mji, aonacho