Page:Swahili tales.djvu/270

This page has been proofread.
250
SULTANI MAJINUNI.

cho chote katika mji hukamata akala. Bassi, bwana, tufanyeje mambo haya?

Akawaambia, nathani ninyi roho zenu, paka huyu hampendi, wataka ni'mue, nami sita'mua paka wangu na hivyo anavyokula vyangu.

Bassi watu wakasangaa, hapana mtu anaothubutu ku'mua, na watu wamekwisha kuliwa na paka. Akakaa njia ya Mnazimoja, tena watu wasipite njia ile; paka akahama njia nyingine, akikamata vilevile.

Wakaenda wakamwambia Sultani, paka anahasiri watu. Akawaambia maneno yenu mimi siyataki, maneno yenu kwangu madogo, wala sisikii maneno haya, wala paka si'mui.

Watu wakahama njia ile wasipate. Akahama njia nyingine akafanya kama yale. Akaambiwa Sultani, amezidi paka, bwana, amekuwa mkali kabisa, hakipiti kitu mbele yake, amekidaka. Akawaambia, paka wangu na hicho anachotwaa changu. Wakahama watu, wasipite njia ile.

Akaona yule Sultani maneno yamekuwa mengi ya watu, aka'mweka mtu mwangoni. Killa mtu atakayekuja hapa kwa mashtaka ya paka, mwambia, bwana hapatikani. Akamwambia, Ee walla, bwana.

Bassi usiku paka huja mjini, akikamata killa apatacho, na ufajiri hurudi akaenda zake kiungani. Hatta mle viungani hamna watu; waliokimbia, wamekimbia, na waliokamatwa, wamekamatwa. Akajongea mbali ndogo mashamba yule paka, akikamata huko watu na nyama, na