Page:Swahili tales.djvu/276

This page has been proofread.
256
SULTANI MAJINUNI.

Na yule mtoto amekaza kule kwimba,

Mamá wee, niulága
Nundá mla watu. (Marra tano.)

Na mamaye akamjibu,

Mwanángu, si yéye
Nundá mla watu. (Marra mbili.)

Akamwacha yule jibwa.

Akamwambia, Ee! siye nunda, yule nunda mkubwa, uwache mwanangu, ukakaa kitako. Akamwambia, mama si jambo la kupatikana mimi la kukaa kitako. Akatoka akaenda zake mwituni.

Akaenda mbali kuliko siku ile, na watumwa wake waliomchukulia chakula. Akaenda akamwona fungo, aka'mua, akamfunga akamkokota, akija naye, hatta alipokoma nussu ya njia akaimba,

Mamá wee, niulága
Nundá mla watu. (Marra sita.)

Mwanángu, si yéye
Nundá mla watu. (Marra tatu.)

Akamtupa.

Akamwambia, mwanangu huachi ukakaa kitako? Utataabika sana, tazama siku hizi mbili umekuwa mweusi. Akamwambia, mama sina buddi na kwenda twaa kisasi cha ndugu zangu. Akamwambia, enenda.

Akaenda katika mwitu mbali zayidi kuliko juzi. Akaenda, akamwona ngawa, aka'mua, akamfunga, aka-