Page:Swahili tales.djvu/278

This page has been proofread.
258
SULTANI MAJINUNI.

mkokota. Alipokuja hatta alipokoma nussu ya njia, akaimba,

Mamá wee, niulaga
Nundá mla watu. (Marra saba.)

Mwanángu, si yeye
Nundá mla watu. (Marra nne.)

Akamtupa.

Akamwambia, utapata wapi nunda huyu naye mbali, nawe humjui alipo, utataabika sana mtoto, uso wako umebadilika kwa siku tatu hizi, utafathali ukakaa kitako. Akamwambia, sina buddi, mama, ya kuenenda. Akamwambia, mama maneno matatu nitapata moja kwa Muungu. Akamwambia, la kwanza mwanangu? Akamwambia, la kwanza ntakufa. Akamwambia, lapili, mwanangu? Ao ntampata nunda, ni'mue. Akamwambia, la tatu mwanangu? Ao ntamkosa nunda nirudi. Bassi matatu haya mama, sitakosa moja kwa Muungu. Akamwambia, mimi mwanangu napenda umpate huyu nunda uje nawe, na roho yangu nimwone, iwe safi. Akamwambia, bassi mama kua heri, naenda zangu.

Akaenda mbali kuliko siku ile, akaenda akamkuta punda milia, aka'mua, akamfunga akamkokota, akaja zake hatta nussu ya njia, akaimba,

Mama wee, niulaga
Nunda mla watu. (Marra nane.)

Mwanangu, si yeye
Nunda mla watu. (Marra tano.)

Akamwacha.

Akamwambia utafathali mwanangu, ukae kitako, roho yangu imefanya khofu, mwanangu. Akamwambia, una