Page:Swahili tales.djvu/28

This page has been proofread.
8
KISA CHA PUNDA WA DOBI.

Akamwambia, hapana neno yalio ndio mazumgumzo ya simba. Akamwambia, twende zetu, bass.

Wakaenda hatta wakafika. Simba alipomwona tu, akamrukia akamkata vipande viwili.

Hatta sungura alipokuja, akamwambia, chukua nyama hiyo ukaoke, wallakini sitaki kitu mimi, ela moyo na mashikio ya punda. Sungura akamwambia, marahaba. Akaenda akaoka nyama mahala mbali, simba hamwoni. Akatwaa moyo ule na mashikio akala yeye sungura, hatta akashiba. Na nyama ngine akaziweka.

Akaja simba, akamwambia, niletee moyo na mashikio. Akamwambia, yako wapi? Simba akamwuliza, kwa nini? Akamwambia, huyu punda wa dobi, huna khabari? Akamwambia, ginsi gani kutoa kuwa na moyo na mashikio? Akamwambia, wewe simba mtu mzima hayakuelei? Kama ana moyo huyu na mashikio, angalikuja tena hapa? Kwani marra ya kwanza amekuja akaona atakuuawa, akakimbia, marra ya pili amekuja tena, bassi kama ana moyo angalikuja? Simba akamwambia, kweli maneno yako.

Bassi kima akamwambia papa, nawe wataka unifanye mimi punda wa dobi, shika njia wende zako kwenu, mimi hunipati tena, na urafiki wetu umekwisha. Kua heri.