Page:Swahili tales.djvu/288

This page has been proofread.
268
SULTANI MAJINUNI.

Akashuka juu ya mti kwa nguvu, akapiga kikorombwe, akajibiwa kikorombwe, akapiga tena kikorombwe marra ya pili, akatega shikio lake—hivi—upande, apate kusikia atakapojibiwa kikorombwe kule, aenende. Akajibiwa kikorombwe marra mbili, akaenda hatta akawakuta wajoli wake wawili juu ya mti. Akawaambia, haya shukeni nunda amekufa. Wakashuka wale mbio, akija zao katta wakimkuta bwana wao, akawaambia, Je! Shindano! Akamwambia, tumefuatana bwana na Kiroboto, nunda amekwisha kufa, bwana, ushuke. Akashuka, akifika chini pale wakikutana wote. Killa mtu akatafuta nguo yake, akavaa. Wakatafuta bunduki zao, wakatafuta yale majamanda, yaliotiwa mabumunda, wakaja, watoto wamekonda kwa siku ile moja.

Wakakaa kitako kule wakala vyakula vyao, wakanywa na maji, wakaenda hatta kule alikoanguka nunda. Kijana alipomwona, akanena, ndiye nunda, ndiye, ndiye! Ah! kweli, bwana, ndiye.

Wakamkokota siku tatu njiani. Hatta wakatoka katika mwitu; roho yake ina furaha, ndiye nunda, akaimba,

Mama wee, ndi yeye
Nunda mla watu. (Marra kumi na moja.)

Mwanangu, si yeye
Nunda mla watu. (Marra nane.)

Ah!——uthia huu, mwanangu, uliokupata! Na watu wa mjini wanataajabu udogo wako, na akili zako kwa kuwa nyingi. Na babaye akamwambia, hapa walipokuwa bass. Usende tena mbele. Akamwambia, baba, mimi sina buddi kwenenda, labuda Mwenyi ezi Muungu amenia-