Page:Swahili tales.djvu/294

This page has been proofread.
274
SULTANI MAJINUNI.

chini sana. Yule mtoto akitazama, roho yake ikamhubiri kuwa ndiye nunda.

Akishuka yule kijana yeye na bunduki yake mkononi, na mkuki wake, hatta akipata nussu ya mlima, akatazama huyu, hapana buddi ndiye nunda. Mama yangu alinambia masikio yake madogo, na huyu yake madogo; alinambia, nunda mpana si mrefu, na huyu mpana si mrefu; alinambia ana mawaa mawili kama ngawa, na huyu ana mawaa mawili kama ngawa. Alinambia mkia wake mnene, na huyu mkia wake mnene; zile sifa zote zake alizoniambia mama yangu, hizi zote ndizo. Akarudi hatta kwa watumwa wake.

Alipofika kwa watumwa wake, akawaambia, na tule sana leo. Wakamwambia, haya bwana, tule. Wakala sana, wakala mikate, na mabumunda, na mkate wa kumimina, na ladu, wakashiba. Wakanywa maji. Akawaambia, mmekwisha? Wakamwambia, bwana, tumekwisha sisi, twakungoja wewe tu. Akawaambia, nami tayari.

Akawaambia lakini leo, akina baba, tusichukue vyombo vyetu kama safari ya kwanza. Vyombo vyetu na vyakula vyetu, na maji yetu, tuweke papa hapa, twende zetu kupigana kule. Kama tumeshinda, tupate kuja kula kulala, kesho twende kwetu, ao tukishindwa, tukimbilie hapa, tupate chakula chetu, tupate kwenda zetu upesi.

Na jua limekuwa alasiri. Akawaambia, haya shukeni, twende zetu. Wakishuka, hatta walipokoma nuss ya mlima, wale watumwa wawili wakafanya woga. Akawaambia, twendeni msiogope, ulimwenguni ni mawili, ni kuwa mzima na kufa. Bassi mwaogopa nini ninyi? Waka-