Page:Swahili tales.djvu/300

This page has been proofread.
280
SULTANI MAJINUNI.

Watu wote wa mjini wakakimbizana kuenenda, wakamkuta yule kijana, anakwimba,

Mama ni lawa kumakoikoi,
Nimbe we mama.
Nilawa kumakoikoi, nimbe we.
Mama wee, niulaga
Nunda mla watu.

Mwanangu, ndi yeye
Nunda mla watu.

Babaye aliposikia mwanawe amekuja, ame'mua nunda, akamwona hakuna mtoto bora katika mwango wake zayidi ya yule. Watu wote walio katika mji, wangwana kwa watumwa, wake kwa waume, wadogo kwa wakubwa, wakaenda kumpukusa. Akapata mali sana, akapendeza sana katika mji, babaye akampenda sana.

Siku ya tatu kuja baba yake akashuka katika enzi, akampa mwanawe. Akamwambia, mimi na mamayo, tupe chakula chetu na nguo, hatutaki illa zayidi, kwani tumekuonea, ndiye kijana mwenyi akili, taabu iliokupata, na mashaka yote, jua lako, mvua yako, kiza chako katika mwitu, watu wakakwambia utakufa, wallakini umerudi mwanangu, bassi mimi pukusa zangu mimi na mamayo, tumekupa hii inchi yako, ndio pukusa zako, mwanangu. Nawe sinene nakukomaza niwie rathi, mwanangu.

Akaamria yule nunda, akachukuliwa, akaenda akatiwa shimoni, akafukiwa sana. Akajenga nyumba juu ya shimo la nunda. Aka'mweka asikari, akamwambia, Killa atakaopita hapa katika njia hii, atoe ada, aweke, na asipotoa