Page:Swahili tales.djvu/318

This page has been proofread.
298
UZA GHALI.

mwambia Sultani, yule kijana wa waziri wako, Ali, amefilisika, watu wakimwuliza—mali yako, Ali, waliyatendani hatta yakaisha upesi? Mali yako ni mengi aliokuachia marehemu babayo, kwani mali yake, ungekuwa na akili, Ali, yangedumu nawe, kwa yale mali kwa kuwa mengi. Na Ali hujibu, akamwambia amwulizaye—asiojua maana, haambiwi maana.

Sultani akanena, kaniitieni Ali, aje ni'mulize maneno haya kweli wanaonena watu ao wanamsingizia. Akaondoka kathi akanena, naam, kweli, Sultani, maneno haya. Akatuma asikari kwenda kumwita kuja wakati wa baraza, na watu pia walipo katika baraza ya Sultani waje, wasikie, maneno haya anaonena Ali kweli ao uwongo.

Hatta Ali akaenda akaazima kanzu mbovumbovu kwa mtu maskini, kwani hapana mtu anayomwamini kumpa nguo zake, na hiyo kanzu Ali apata kwa tafáthali na kwa angukia.

Hatta akaenda mwangoni mwa Sultani, na baraza imejaa tele watu, na Sultani amekaa kitako. Sultani akaondoka, akamwita—Ali! Akaitika—Lebeka. Akamwambia, Ali, nimesikia maneno kama mali yako yamefilisika, na wewe huwajibu watu wanaokuuliza, huwaambia—Asiyojua maana, haambiwi maana.

Akamwambia—Na'am Bwana, mali haya naliyapiga mafungu manne, fungu moja nalitia baharini, fungu moja nalipiga moto, fungu moja nalikopesha wala sitalipwa, fungu moja nimelipa deni wala sijaisha kulipa.

Sultani akamwambia—Ali, uza ghali, si uza rakhisi. Ali akamwambia—Ee Walla, hababi. Akatoka, akaenda zake.