Page:Swahili tales.djvu/32

This page has been proofread.

SULTANI DARAI.


Aliondoka sermala, akaenda kuoa mke. Akakaa na mke wake miaka mingi, hatta akapata kijana manamke. Yule mkewe akapatikana na ugonjwa hatta akafariki dunia, akakaa na mtoto wake mdogo.

Akanena, mimi hapo ndipo manamume, ni mtu wa kwenda kazini, na kijana changu nalionaye ni mdogo, afathali nitafute mke, nioe, illi maksudi apate kulea huyu mtoto wangu; kama sikuwa na mke mtoto wangu atathii.

Nduguye akamwambia, astahili uoe, kwani wewe ni mwanamume, mtu mzima tena, na mtoto mdogo, bassi hutaweza, afathali uoe mke, akaaye na mtoto wako, na weye mwenyewe upate kwenda kazini. Akamwambia, vema, mashauri yako mema, bassi weye walionipa shauri hili, nifanyie shauri jema, ni mke upendaye, umwonaye mwema, nami nikubali. Akamwambia, yuko mwanamke mmoja jirani yangu, alikuwa mwanamke wa marehemu Salih, bassi roho yake nimemwona kuwa mwema, kwani alikaa sana na mumewe, sikusikia kugomba, bassi sijui wewe na nasibu yako, lakini mimi nimemwona mwanamke