Page:Swahili tales.djvu/324

This page has been proofread.
304
UZA GHALI.

mimi katika roho yangu. Akamwambia, sijui, rafiki yangu, linalokuja kwa Muungu lote jema.

Ali akasema, akibisha sasa nitamwitikia, akiniua na aniue, akiniacha bass, wala sina buddi illa kumwitikia.

Akabisha waziri, akamwita—Ali! Akamwitikia, lebeka, nani weye unayokuja niita usiku, na usiku huu umekuwa wa manane? Akamwambia, ni mimi, nina shughuli nawe. Akamwambia, sikujui weye, bwana, uliokuja. Akamwambia, usiogope, nimekuja kwita kwa kheri, sikuja kwita kwa shari. Akamwambia, bwana, kuniita kwako, ndiko unisaburi hatta assubui. Waziri akamwambia, hapa nilipo, siwezi kukusaburi hatta kwa dakika moja, hivyo unavyonena ndani naona unakawia. Tafáthali, Ali, toka nje, usikie neno langu nalikwitia.

Akamwambia—Ee Walla, bwana, naweka sikio langu katika mwango uniambie jina lako, ndiyo nitakapoamini kutoka, kwani ndipo nimekwisha kukujua.

Akaenda waziri akamwambia, ni mimi, Waziri wa Sultani, tafáthali toka, nna maneno nawe kwambia na maneno haya kwa faragha. Ee Walla, bwana wangu. Akaenda Ali akamwambia rafiki yake, yule maskini, nimekuja kwitwa na waziri wa Sultani, akataaye witwa hukataa aitiwalo.

Akamwambia, rafiki yangu enenda, labuda kuna kheri nawe. Akifungua mwango Ali akimwona waziri na mtumwa wake mmoja. Akamwambia, Bwana, masalkheiri. Akamwambia, marahaba, Ali, tuondoke, twende zetu kwangu. Akamwambia—Ee Walla, Bwana.

Yule waziri na Ali wakafuatana hatta nyumbani kwake. Waziri akipanda darini, saa saba ikipiga ya usiku, Waziri akamwita mjakazi wake, Mrashi! Aka-