Page:Swahili tales.djvu/34

This page has been proofread.
14
SULTANI DARAI.

mwema, naye ana mtoto mmoja mwanamke, alioachiwa na marehemu mumewe.

Akamwambia, bass, enenda kamtake, usikie majibu atakayokwambia, nawe kesho uje unijibu kwa wakati ntarudi kazini. Akaenda, akamwambia yule mwanamke, kuwa manamume amekuja kukutaka, nawe nijibu utakalonambia, nami nende hamjibu. Akamwambia, mimi kumkataa siwezi, kwani hapo nilipo ni mjani, nami na mtoto, bassi nipatapo mume naona raha zayidi. Akamwambia, vema, nitakwenda kumjibu.

Akaenda hatta kwa nduguye. Akamwambia, nimekuja kukujibu majibu yako, walionituma jana. Mwanamke nimemwambia, hakunijibu maovu, amenipa maneno mema ya sharia yenyi njia. Akamwambia, bassi mimi ntakupa nguo na mahari umpelekee, na ukienenda mwambie, haya mahari yako, na hizi nguo zako, kama una neno lingine nambie nikamjibu. Mwanamke akamwambia, mimi sina neno, maadamu yamewasili mahari na nguo, sina jambo nafsini mwangu lingine la zayidi. Nami nakwambia mume wangu na aje siku ya Juma tano.

Akaenenda kumjibu, nimempelekea mwanamke nguo na mahari, nimempa, hamwuliza, una neno zayidi? Akaniambia, sina neno nafsini mwangu zayidi, neno lake ni moja alioniambia, mwache mume wangu aje siku ya juma tano, bass! Akamwambia, Juma tano si mbali, tukijaliwa na Muungu, ni leo juma 'nne hatta kesho imekuwa juma tano. Akamwambia, fanya shughuli zako tayari. Akamwambia, mimi sina shughuli tena, shughuli zangu zimekwisha, ni tayari mimi na mwanangu, lakini weye ndugu yangu enenda kamwambia mke, nao kwao