Page:Swahili tales.djvu/354

This page has been proofread.
334
HASSIBU KARIM AD DINI.

Akawaambia, jina lake, Hassibu karim ad dini. Wakamwambia, heri.

Akatiwa chuoni kusoma, alipokwisha soma, akatiwa kiwandani kushona nguo, asijue, akatiwa kufua fetha, asijue, killa kazi anayofundishiwa hajui. Mamaye akanena, bassi, kaa kitako, mwanangu. Akakaa kitako akila na kulala.

Akamwambia, baba alikuwa na kazi gani? Akamwambia, alikuwa tabibu mkuu sana. Akamwambia, viwapi vyuo vyake vya utabibu? Akamwambia, siku nyingi zimepita, katezame ndani, kana viko. Akaenda, akatezama, akaona vimeliwa na wadudu imesalia gombo moja, akatwaa, akasoma, akaona dawa zile zote.

Hatta siku hiyo wakaja jirani zake wakamwambia mamaye, utupe sisi huyu mtoto tukaende naye kuchanja kuni. Nao, wale watu wanne, kazi yao kuchanja kuni, wakija, wakiuza mjini. Nao hupakia kuni juu ya punda. Mamaye akawaambia, vema, kesho nitamnunulia punda, mfuatane nyote.

Assubui mamaye akamnunulia punda, wakaja wale watu, wakafuatana naye kazini. Wakaenda, wakapata kuni nyingi, wakaja nazo mjini kuza, wakagawanya fetha.

Na siku ya pili wakaenda tena, na siku ya tatu, na siku ya nne, na siku ya tano, na siku ya sita. Hatta siku ya sabaa, walipokwenda, kukatanda wingu, ikanya mvua, wakakimbia kujificha chini ya jabali.

Yule Hassibu amekaa mahala pekeyake. Akatwaa