tayari. Akikwambia, tu tayari, njoo niite twenende wakati umekuwapo naliokwambiwa kuenenda.
Akaenda hatta kwa mke akamwambia, mumewo akusalimu, nanyi huku m tayari? Bwana harrusi ataka kuja. Akamwambia, siye tu tayari twamngoja yeye kuja, na wakati unapita, enenda mwambia upesi aje.
Akaenenda mbiombio akamkuta nduguye akisimama mlangoni, yu tayari kutaka kutoka. Akamwambia, mkewo salaam. Akamwambia, Je! habari gani? Akamwambia, hakuna habari illa wewe upesi unakwitwa, nao huku wa tayari wakungoja wewe kuenenda, haya, upesi, wakati unapita. Wakaondoka, wakitoka nyumbani, wakaenda zao hatta wakifika nyumba ya mkewe, akasimama nje. Akaingia yule nduguye, akamwambia, haya waanawake, bwana harrusi amekuja ataka kuingia nyumbani. Akamwambia, ruhusa na apite. Akaenda.
Wakakaa nyumbani kwake, yee na mkewe na mwanawe na yule mtoto wa mkewe, hatta muda wa siku saba kwisha. Akamwambia, mke wangu. Akamwambia, lebeka bwana. Akamwambia, kesho siku alhamisi nitakwenda kazini, kaa sana na mwanao naye mtoto mdogo. Hatta ussubui walipokucha, akaenda zake kazini.
Mwanamuke huku nyuma akapika chakula akawapa sehemu zao watoto, killa mtu mbali mbali, yule mwanawe akampa wali mwema, na yule mwana wa mumewe akampa ukoko walioungua.
Hatta athuuri akija babaye, Pakua, bibi, chakula. Mwanamke akaenda jikoni akapakua chakula, akaenda kumwandikia mumewe, akampa maji kunawa. Akamwambia, Waite watoto, tule chakula. Mwanamke akamwambia,