Page:Swahili tales.djvu/360

This page has been proofread.
340
HASSIBU KARIM AD DINI.

juu ya kitanda, na kile ndicho kitanda cha Sultani, anachokaa. Wakataka kumwua, akawaambia, mwacheni, msimwue, niwekeni kitini, waka'mweka juu ya kiti.

Akawaambia, mwamusheni polepole, wakamwamusha. Akaondoka, akakaa kitako, akaona nyoka wengi, wamemzunguka, akamwona yule mmoja mzuri sana, amevaa nguo za kifaume.

Akamwuliza, wewe nani? Akamwambia, mimi Sultani wa nyoka, na hii nyumba yangu; akamwuliza, na wewe nani? Akamwambia, mimi Hassibu karim ad dini. Watoka wapi? Akamwambia, sijui ninapotoka wala ninakokwenda. Akamwambia, starehe; akawaambia asikari wake, enendeni mkalete matunda yote mwituni, tumkerimu mgeni.

Wakaenda, wakaleta kulla tunda, waka'mwekea mbele sinia nzima, wakamwambia kula. Akala hatta akashiba, wakampa maji, akanywa. Bassi, akakaa kitako, wakazumgumza.

Yule Sultani wa nyoka akamwuliza Hassibu, nipe kisa chako, toka ulipotoka kwenu hatta leo. Akampa kisa chote kilichompata njiani hatta akafika pale.

Naye Hassibu karim ad dini akamwuliza Sultani wa nyoka, unipe kisa chako nawe, nipate kujua. Akamwambia kisa changu kikubwa sana.

Akamwambia, nalikaa zamani moja, tukaondoka hapa kwenda jabali Al Káf, kwenda kubadili hawa. Nikakaa hatta siku moja nikamwona mtu akija nikamwuliza, watoka wapi wee? Akaniambia, mimi natoka mjini kwetu, ninapotea katika barra. Nikamwambia, weye mtoto wa nani? Akaniambia, mimi jina langu Bolukia, na baba