Page:Swahili tales.djvu/386

This page has been proofread.
366
MWEWE NA KUNGURU.

Sultani akamwuliza, akamwambia, wenzangu wamenipiga, wamenitoa mji kwa sababu naliwaambia kweli, mfuateni mwewe, ndio Sultani, wakanipiga. Sultani ya mwewe akamwambia, kaa kitako hapa.

Akakaa kitako siku nyingi. Hatta siku moja wakaenda kanisani, nayee wakamchukua, wakasali pamoja, hatta walipotoka, wakamwuliza, sisi na ninyi, nani anaabudu sana Muungu? Akawaambia, ninyi.

Akakaa kitako wakampenda sana. Hatta siku kuu yao ikikaribia, akatoka usiku, akaenda, akawaambia wenziwe, kesho watakwenda kanisani wote, njooni nje ya mlango wa kanisa, mutie moto. Wale wakatoka, wakaenda kutafuta kuni na wangine wakachukua moto.

Hatta assubui wakaenda zao kanisani, asisalie mtu katika mji, ela yule mzee kunguru. Wakamwambia, kwa nini huenendi kanisani leo? Akawaambia, tumbo linaniuma sana. Wakamwambia, bass. Akaenda, akawaita wenziwe. Akawaambia, wamekwisha kuingia kanisani wote.

Wakaenda wale, wakatia kuni katika mlango wa kanisa, na wangine wakatia moto. Moto ukawaka. Wakaona moshi waingia ndani ya kanisa, wakakimbia madirishani na wangine wakafa wengi sana na Sultani pia akafa. Kunguru wakatwaa mji.

Wale waliobaki mwewe wakawakimbia kunguru hatta leo.