Page:Swahili tales.djvu/40

This page has been validated.
20
SULTANI DARAI.

mwanamke, wakakaa kitako kula, wakiisha wakanawa mikono, wakaondoka.

Akamwambia, mke wangu, niletee tambuu. Mbona tumbako hamna, funua chini ya mchago, akamwambia, nalifahamu kuweka jana tumbako, bassi tezama uniletee. Akaenda mwanamke, akafunua mchagoni, tumbako asione. Akamwambia, bwana. Akamwambia, lebeka, bibi. Mbona nimefunua mchagoni, tumbako sikuiona? Akamwambia, tezama sana, ela tartibu, ukitezama kwa harraka, hutaona kitu. Ee, bwana, natezama kwa taratibu, na tumbako siioni. Akamwambia, tezama illa miguuni. Akafunua kitanda yule mwanamke asione tumbako. Akamwambia, Ee, bibi wee, labuda umekwenda kwa harraka hapo kitandani, tumbako nathani umeyangusha chini. Akamwambia, bwana chini haikuanguka. Akamwambia, kama husadiki nitatwaa taa nimulike hapa chini ya mvungu, kama iko tumbako yako ntaiona. Bassi mulika upesi, nami nimekwisha unga tambuu, nangojea, hiyo tumbako tu, unaitafuta kutwa kamma sindano, ndio huioni, nawe ungeiona sembuse hiyo tumbako, nalo jino zima si kipande kidogo. Ah! Bwana siwezi, njoo tafuta mwenyewe nami huku. Siji nimechoka, tafuta uniletee bass, ufunue mikeka yote ukatezame; hiyo tumbako, bass, imekwenda wapi? Eee! mke wangu, nimesahau iko ndani ya mfumbati kitanda kidogo. Ah! bassi wee, waliotaka kuniathibu, nawe wajua tumbako walipoweka. Walitaka kuniathibu mimi, mwana wa mwenzio. Akitwaa chini ya mfumbati tumbako, akampelekea. Shika tumbako yako, una wazimo wako, hatta mtu wali hujaisha kumshuka matumboni, unaingia ukiniathibu. Ah! mke wangu, nimechoka, nami