Page:Swahili tales.djvu/404

This page has been proofread.
384
PEPO NA MTOTO WA SULTANI.

Akamwambia, tufanyeje? Akamwambia, njoo unifungue, akamfungua. Akamwambia, sasa fungua chumba cha mali, mimi nitameza killa kitu, na baba yako akija akaenda kuwaita watu kuja kutula, na akija, atakwambia, twendee kuni, useme mimi sijui kazi hiyo, atakwenda yeye pekeyake; akija nazo atateleka sufuria kubwa, atakwambia, chochea moto, mwambia, siwezi, atakwenda mwenyewe kuchochea moto, ataleta samli nyingi, ataitia ndani ya sufuria, hatta ikipata moto atafunga pembea, atakwambia, panda ucheze, mwambia, sijui mimi kucheza mchezo huu, panda wewe mwenyewe nikuangalie kwanza, na mimi nipate kufanyiza kana weye, akipanda yeye kukuonyesha, msukume ndani ya sufuria ya samli ya moto, uje zako mbio, na miye nitakwenda kukungoja chini ya mti huko njiani.

Farasi akakimbia, akamwacha mtoto pekeyake. Hatta alipokuja baba yake, akamwambia, kesho twendee kuni. Akamwambia, mimi sijui kazi hiyo. Akamwambia, bass, kaa kitako. Akaenda mwenyewe pekeyake, akaleta kuni nyingi. Naye amekwisha waambia watu, kesho nna karamu, njooni. Akaja akatoa sufuria akateleka, akamwambia, tia kuni, akamwambia, sijui mimi. Akamwambia, kaleta samli, akamwambia, siwezi kuichukua, sina nguvu. Akaenda mwenyewe, akaichukua, akaitia ndani ya sufuria, akatia moto. Akamwambia, chochea, akamwambia, sijui kuchochea moto.

Akamwambia, umewona mchezo wa kwetu? Akamwambia, sijauona bado. Na samli imepata moto sana. Akafunga pembea, akamwambia, panda hapa, nikuonyeshe.