Page:Swahili tales.djvu/42

This page has been proofread.
22
SULTANI DARAI.

nalisahau, bassi kumekuwa wakati wa usiku, waita watoto walale, ondoka kafunga mlango. Watoto wakaingia kwao chumbani kulala, na baba zao akaenda zake kulala.

Hatta ussubui walipokucha, akamwaita, Mke wangu. Akamwambia, lebeka, bwana. Naenda zangu kazini, mtazama mtoto asitoke nje na acheze hapa ndani uwanjani na nduguye. Akamwambia, Ee walla, bwana. Akaenda zake kazini.

Mwanamke akapika chakula akawaita, Watoto! Lebeka, Mama! wakaja wote wawili mbio. Yule mtoto wa mumewe akamwambia, miye, mama. Ah! nalikwitwa mimi mama yako, nalikuzaa lini? Mamako yule amekufa kule, mimi namwita mwanangu, naliomzaa mwenyewe. Yule kijana akazunguka nyuma, akakumbuka, akalia sana, hatta yule mwenziwe akamwambia, dada, unalia nini?

Akamwambia, mimi si dada yako, mama yako ameniambia, mamako yule amekufa, mimi si dada yako, mimi kuwa dada yako ningepewa ukoko wa wali tena ulioungua? Wewe ukapata wali mwema, na kitoweo kukupa, mimi hala ukoko mkavu ila kuwa na mchuzi sababu mimi sina mama, bass; mimi si dada yako. Yule kijana akaondoka akamwita, Mama! Mwanangu! Mbona yule dada amezunguka nyuma analia, mama, umemtendani? Ah! mimi, yule si mwanangu, nalikuzaa pekeyako. Ah! si mtoto wa baba? Akiwa mtoto wa babayo, bassi nimtendeni? Nimtie katika mboni ya macho, utakapojua kweli kamma huyu ni nduguyo. Uss, nyamae si nene, kamwita mle chakula. Akamwambia, dada unakwitwa. Nani ananiita? Unakwitwa na mama. Unanikufuru wewe, sina mama mimi,