Page:Swahili tales.djvu/420

This page has been proofread.
400
AO RATHI, AO MALI.

niletee machela. Akaenda mtumwa wake marra hiyo akarejea na machela na watu wanne, wakamchukua. Akamtia manamke, akamwambia mtumwa wake, piga bunduki, wapate kuja jamaa yote. Akapiga bunduki, wakaja watu wenzi wake, wakamwambia, una nini, kijana cha mfalme? Akamwambia, una baridi, nataka kwenda zangu mjini. Wakachukua nyama iliopata, wakaenda zao. Na kijana cha mfalme ameingia ndani ya machera, yeye na yule kijana manamke. Na wale wenziwe hawana habari.

Wakaenda hatta mjini kwao, wakafikia nyumbani kwake. Akamwambia mtu—enenda kamwambia mama na baba, nna homa leo, nataka uji upesi, waniletee. Wakafathaika mamaye na babaye, akapikiwa uji, akapelekewa.

Na babaye akaenda na mawiziri yake wakaenda kumtezama. Hatta usiku mamaye akaenda na watu wake kumtezama.

Hatta siku ya pili akatokea nje, akaenda, akamwambia mamaye na babaye, nimeokota kijana manamke nataka mnioze, walakini hana mkono moja. Wakamwambia, wa nini? Akawaambia, nataka vivyo hivyo. Na yule Sultani ampenda sana mwanawe mmoja tu, akafanya harusi, wakamwoza.

Watu wakapata habari mjini, mtoto wa Sultani ameoa kijana manamke, hana mkono moja.

Wakakaa kitako hatta mkewe akachukua mimba, akazaa mtoto manamume, wakafurahi mno wazee wake.

Yule kijana cha Sultani akasafiri, akaenda kutembea katika miji ya baba yake.

Huko nyuma akatokea yule ndugu yake manamume, hana kitu cha kutumia, anakwenda akiomba. Hatta siku moja, akasikia watu wanazumgumza—kijana cha mfalme