Page:Swahili tales.djvu/428

This page has been proofread.
408
AO RATHI, AO MALI.

Wakaenda, wakikaribia, akatezama durabini yule manamke, akamwona mumewe, na baba ya mumewe, na watu wengi, na yule nduguye yumo. Akawaambia watu, fanyeni vyakula upesi. Wakafanyiza, wakaandika meza. Wakafika, wakakaribishwa, wakaingia ndani, wakamwuliza habari. Akamwambia, njema. Akawaambia, kaleni chakula, natoka mbali mimi, mkiisha chakula, niwape habari yangu,

Wakala chakula, hatta walipokwisha, akawaambia, toka mwanzo alipozawa, yeye na nduguye manamume, hatta yakaisha yote, kama yalipokuwa. Yule kijana cha mfalme akaenda kumkamata mkewe, wakalizana sana, na waliopo wote wakalia, wakajua kuwa nduguye manamume si mwema.

Mfalme akamwuliza, tumfanyieje nduguyo mwanamume? Akamwambia, mtoeni mji tu. Akakaa na mumewe hatta hatima kwa furaha.