Page:Swahili tales.djvu/434

This page has been proofread.
414
TUMBAKO.

Wakaenenda hatta walipofika nyumbani. Akamwambia, bwana niambie neno la tatu. Akamwambia, tua. Akamwambia, nina furaha mno kwa yale maneno mawili ulioniambia, niambie la tatu, nipate kutua.

Akamwambia, mtu akikwambia, njaa ni bora kuliko shiba, usimsadiki.

Akamwambia, jitenge, bwana, nilitue. Akaliinua juu ya kitwa, akalipomosha. Mwenyewe akamwambia, a-a-a umenivunjia sanduku yangu!

Akamwambia, na mtu akikwambia, imesalia bilauri moja katika sanduku hii haikuvunjika, nawe usimsadiki.


TUMBAKO.


Tumbako ilipoingia katika ulimwengu, walipoiona wenyi akili waliitwaa wakainuka, waandamizi wenyi akili waliitwaa, wakaivuta, wakaangalia moshi wake. Wapemba wapumbavu walithanya, ni vyakula, wakaitwaa, wakaila.