Page:Swahili tales.djvu/44

This page has been proofread.
24
SULTANI DARAI.

mamangu yule amekufa, mwenyi mama wewe tu. Hupewa wali mwema ukila, bassi, uende kwa mamayo. Ee dada, si fanya hasira, twende zetu tukale. Mimi huko siendi, nileteeni wangu papa hapa.

Akaondoka, akaenenda, akamwita mama. Akamwitikia, mwanangu yu wapi nduguyo? Akamwambia, mimemwita, hataki kuja, akaniambia nipelekee wali kuko huko. Akamwambia, yuko wapi? Yuko nyuma uani. Chukua, mpelekea. Akachukua yule kijana, akaenda akampelekea. Dada, dada, wali huu nimepewa kukupa. Akamwambia, wache hapa nitakula. Akiweka wali chini, akashika njia kwenda zake.

Je! umempa wali nduguyo. Nimempa hajala na akaniambia, weka chini, nami nikaweka. Bassi kaa kitako, ule wali wako. Hatta akala, akaisha.

Kamtezame nduguyo amekwisha kula wake. Naye akaenda akamkuta amenamia chini, na machozi humtoka, akumbuka yale yaliotendwa na yule mke wa babaye. Akamwita, dada yangu, usilie sana, kitwa hicho kitakuuma, afathali ule wali. Akamwambia, roho yangu ina hasira, nami nakumbuka ulimwengu rohoni mwangu, wali haupiti, nami njaa ninayo. Kwa nini, ndugu yangu? Akaambia, hivyo tu. Akatwaa ule wali akampa mbuzi.

Marra babaye akaja, akapiga hodi! Mke akaitika hodi! Karibu bwana! Akamwambia, habari ya pwani? Kwema, jua kali, nipe maji kidogo ninywe. Akapewa maji, akanywa. Akamwita, Bibi! Lebeka, bwana!